Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakizima moto uliowashwa na
wananchi katika Ofisi ya Mtendaji, Kata ya Kizwite, Sumbawanga, Rukwa
juzi baada ya kutokea kutoelewana wakati wa kuhesabu kura.
Wasimamizi wa
uchaguzi katika maeneo mbalimbali nchini, jana waliendelea kutangaza
matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambayo yameonyesha vyama vya
upinzani vikichomoza na ushindi katika sehemu ambazo awali, hazikuwa
ngome yake.
Katika mamlaka ya mji mdogo wa Usa River, Arumeru
mkoani Arusha, Chadema kimepata ushindi katika mitaa mitano ya Mjimwema,
Magadirisho, Manyata, Magadini na Kisambare wakati CCM imeshinda mitaa
minne ambayo ni Ngaresero, Chemchem, Mlima-Sioni na Nganana.
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari
alisema ushindi huo ni mkubwa kwani kabla hawakuwa na uongozi wowote
katika vijiji lakini sasa wamechukua vijiji 29 na zaidi ya vitongoji
100.
CCM kwa upande wake, kimeendelea kumiliki Serikali
za Vijiji vya Wilaya ya Longido, baada ya kushinda vitongoji 165 kati
ya 168 na vijiji 47 kati ya 49. Mkuu wa Wilaya ya Longido, James Millya
akizungumza jana alisema katika Mji wa Namanga, CCM imeshinda mitaa
mitano, Chadema na CUF mtaa mmojammoja.
Katika vijiji vilivyopo pembezoni mwa Manispaa ya
Shinyanga, msimamizi wa uchaguzi, Festo Kang’ombe alisema kati ya vijiji
17, CCM kimeshinda vijiji 14 na Chadema kimoja. Kang’ombe alisema kati
ya vitongoji 84 katika manispaa hiyo, CCM imeshinda 65 na Chadema
vitongoji 18.
Alisema uchaguzi utarudiwa kesho katika Mtaa wa
Katunda baada ya kushindwa kufanyika juzi kutokana na mkanganyiko wa
picha na majina ya wagombea. Katika Manispaa ya Mtwara (Mikindani), Msimamizi
wa Uchaguzi, Lembakisye Shimwela alisema CCM ilipita bila kupingwa
katika mitaa 11 kati ya 111.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, CCM
ilishinda vijiji 136 kati ya 197 na upinzani umeshinda vijiji 61.
Tandahimba CCM imeshinda vijiji 102, upinzani vijiji 38 na Newala CCM
imeshinda vijiji 120 kati ya 155 na upinzani vijiji 23. Katika Wilaya ya Masasi, CCM imeshinda mitaa 171
kati ya 189 na upinzani mitaa 12. Wilayani Nanyumbu, CCM imeshinda
katika vijiji 70 kati ya 93 na upinzani umeshinda vijiji 12.
Mkoani Kagera katika Wilaya ya Muleba, kati ya
vijiji 164 CCM imeshinda 89 dhidi ya Chadema (70) na CUF (5), vijiji
viwili vya Goziba na Rulanda uchaguzi haujafanyika. Katika vitongoji 460
CCM imeshinda 298, Chadema (153) na CUF (9).
Dar es Salaam
Iringa, Njombe na Pwani
Katika Manispaa ya Kinondoni, CCM imepeta kwa kushinda viti 133
vya uenyekiti, Chadema viti 34 na CUF 16 kati ya mitaa 197. Mitaa 13
haijafanya uchaguzi. Ofisa uchaguzi wa Manispaa ya Kinondoni, Valence
Urassa alisema mitaa miwili haikufanya uchaguzi na 13 uchaguzi wake
umeahirishwa. Katika Manispaa ya Temeke, habari zinasema CUF imeubuka
mshindi katika mitaa ya Butiama na Mbagala na CCM imepata ushindi katika
mitaa ya Matumbi, Njaro, Maganga, Maji Matitu, Kijichi, Mgeni Nani,
Rangitatu na Vetenari. CCM imeshinda katika mitaa minne kati ya mitano ya
Kata ya Ilala na mtaa mmoja haukufanya uchaguzi. Buguruni yenye mitaa
sita, uchaguzi huo ulifanyika katika mitaa minne na CCM imeshinda mmoja
na CUF mitatu. Katika Kata ya Ukonga yenye mitaa mitano, uchaguzi
huo ulifanyika kwenye mitaa miwili na CCM imepata kiti kimoja na CUF
kimoja. Chadema iliibuka mshindi kwenye Mtaa wa Mongo la Ndege.
Morogoro
Matokeo mengine ni ya mkoani Morogoro. Katika Kata
ya Kiwanja cha Ndege yenye mitaa 13, CCM imeshinda mitaa 10. Chadema
imeshindi mitaa miwili na CUF mmoja. CCM pia imechakua mitaa 12 ya Kata ya Sabasaba na
katika Kata ya Lukobe ambayo ina mitaa minane, CCM imeshinda katika
mitaa mitano na Chadema mitatu. Katika Mtaa wa Lukobe Juu, Chadema imepata kura
188 na CCM kura 166 wakati katika Mtaa wa Tushikamane, CCM imeshinda kwa
kura 328 dhidi ya 299 za Chadema. Katika Mtaa wa Majengo Mapya, CCM imepata mitaa
376 huku Chadema ikipata mitaa 308 wakati katika Mtaa wa Tuelewane, CCM
imeshinda mitaa 295 na Chadema mitaa 114. CCM pia imeshinda mitaa minane
katika Kata ya Mafisa.
Kilimanjaro
Katika Kata ya Kahe Mashariki, Kilimanjaro yenye
vijiji sita, CCM ilipata vijiji vinne na NCCR Mageuzi viwili wakati
katika mji mdogo wa Bomang’ombe wilayani Hai, Chadema ilipata viti tisa
dhidi ya vinane vya CCM.
Mwanza
Katika Kata ya Ilemela CCM imeshinda mitaa 106 na
Chadema 62 na katika Wilaya ya Nyamagana Chadema imeshinda viti 70, CCM
viti 96, ACT kiti kimoja na CUF saba.
Iringa, Njombe na Pwani
Katika Manispaa ya Iringa, Kaimu Mkurugenzi wa
Manispaa hiyo, Erasto Kiwale ametangaza CCM kushinda mitaa 126 sawa na
asimilia 69.6, Chadema mitaa 54 sawa na asimilia 29.8 na CUF mmoja.
Kiwale alisema uchaguzi katika mitaa tisa ambayo haikufanya juzi,
utafanyika leo.
Mkoani Njombe, CCM imeshinda mitaa 54 na Chadema
imepata mitaa 28 Mji wa Njombe. Katika vijiji 108, CCM imeshinda 94,
Chadema vijiji sita na NCCR Mageuzi kimoja.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa CCM, imeshinda kwenye vijiji 64, Chadema tisa. Vingine havikufanya uchaguzi. Wilayani Wanging’ombe ambako kuna vijiji 108, CCM imeshinda
vijiji 94, Chadema saba na vingine saba havikufanya uchaguzi. Wilayani
Makete matokeo hayajakamilika lakini CCM imeshinda vijiji 34.
Mkoani Pwani
CCM wameendelea kuufanya mkoa huo kuwa ngome yake kwa kupata ushindi mkubwa katika sehemu nyingine. Katika Kata ya Dimani, Rufiji imeshinda vitongoji 11 na CUF viwili.
Mkoani Pwani
CCM wameendelea kuufanya mkoa huo kuwa ngome yake kwa kupata ushindi mkubwa katika sehemu nyingine. Katika Kata ya Dimani, Rufiji imeshinda vitongoji 11 na CUF viwili.
Kata ya Mwambao Chadema kimeshinda katika Kijiji
cha Mchungu. Jimbo la Mafia CCM ilishinda vijiji 19 kati ya 23 na CUF
imeshinda katika vijiji vinne.
Kibaha Mjini, CCM imeshinda katika mitaa 62 kati
ya 73 iliyopo na upinzani umeshinda katika mitaa 10. Kibaha Vijijini
kwenye vijiji 32, CCM ilishinda vijiji 31 ikiwamo mitaa 10 ilikopita
bila kupingwa.
Bagamoyo Mjini, CCM imeshinda mitaa 57 kati ya 60
na CUF imechukua mitaa mitatu. Kwa upande wa vijiji wilayani humo, CCM
ilishinda vijiji 67 kati ya 75 na vinane havijafanya uchaguzi. Wilayani
Kisarawe CCM imeshinda vijiji 57 kati ya 66 na upinzani imeshinda tisa.
Uchaguzi haukufanyika katika Wilaya ya Mkuranga kutokana na sababu mbalimbali hadi Jumapili ijayo.
Tanga na Singida
Jijini Tanga CCM kimeshinda kwa asilimia 63 ikiwa
na wenyeviti wa mitaa 118, kikifuatiwa na CUF iliyopata asilimia 33 sawa
na wenyeviti 60 na Chadema viti viwili.
Msimamizi wa uchaguzi katika Wilaya ya Pangani,
Zabib Shaaban alisema CCM imeshinda katika vijiji 23 ikifuatiwa na CUF
kilichopata vijiji saba na Chadema vijiji viwili.
Hata hivyo, uchaguzi utarudiwa Jumapili katika
mitaa minane kutokana na kutofanyika juzi baada ya kutokea dosari
mbalimbali zikiwamo za ukosefu wa karatasi.
Katika Wilaya ya Handeni, CCM kimeshinda vijiji 88 kati ya 91 na upinzani umeambulia patupu. Uchaguzi katika vijiji utarudiwa.
CHANZO: MWANANCHI
Katika Manispaa ya Singida CCM kimeibuka kidedea baada ya kuzoa nafasi zote 50 za uenyeviti wa mitaa.
Msimamizi wa uchaguzi wa manispaa hiyo, Joseph
Mchina alisema katika vitongoji 90 CCM imeshinda vitongoji 81 na CUF
kimeshinda vitongoji vinane. Chadema kimoja.
No comments:
Post a Comment