Elvis Mushi akisoma matokeo ya utafiti huo wa Twaweza
Dar es Salaam. Uungwaji mkono wa Chama cha Mapinduzi (CCM) umeongezeka mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana, utafiti umebaini.
Takwimu za utafiti huo zinaonyesha kuwa uungwaji mkono wa CCM umeongezeka mpaka asilimia 54 kutoka 47 za mwaka jana.
Utafiti huo uliofanywa na Twaweza, umeonyesha kuwa
chama hicho kinaungwa mkono zaidi na watu wazima wenye zaidi ya miaka
35, huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikiungwa mkono na
vijana chini ya miaka 35.
Akiwasilisha matokeo ya utafiti huo, mtafiti wa
Twaweza, Elvis Mushi alisema asilimia kubwa ya wapigakura vijana
hawajihusishi na chama chochote cha siasa.
Mushi alisema kama mtawanyiko huo wa uhusiano wa
chama na makundi ya umri utabaki kama ulivyo kwa kipindi kirefu, utatoa
‘faida za kidemografia’ kwa upinzani hapo baadaye, hasa kwa sababu ya
ongezeko la kasi la idadi ya watu.
Utafiti huo unaonyesha asilimia 44 ya vijana chini
ya miaka 35 wanaiunga mkono CCM, wakati asilimia 34 ya vijana wa umri
huo wanakunga mkono Chadema.
Asilimia 60 ya wenye umri kati ya 35 – 50 wanaiunga mkono CCM wakati asilimia 24 wanaipenda Chadema.
Ushindani CCM balaa
Ripoti hiyo inabainisha kuwa ushindani ndani ya
CCM umeongezeka ikilinganishwa na miaka iliyopita na kuwa makada wengi
wamejitokeza hadharani kutangaza nia.
Baadhi ya watu waliojitambulisha kuwa ni wanachama
wa CCM, waliulizwa ni nani anapaswa kupeperusha bendera ya chama hicho
kwenye uchaguzi ujao na asilimia 42 ya waliohojiwa walisema hawana
uhakika, ikiwa na maana wanaweza kuhamia popote.
Baadhi ya wahojiwa (asilimia 24) hawakutaja jina
lolote, lakini walieleza kuwa watamuunga mkono mgombea yeyote
atakayependekezwa na CCM.
Wale waliotaja majina ya watu, asilimia 17
walimtaja Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akifuatiwa na Waziri
Mkuu Mizengo Pinda (asilimia 14). Lowassa ameonekana kumzidi Pinda mwaka
huu tofauti na mwaka 2012 ilipokuwa kinyume chake.
Ripoti hiyo inabainisha kuwa hakuna mgombea mwingine aliyepata zaidi ya asilimia 10 mwaka huu ambao ni Bernard Membe asilimia sita, Dk John Magufuli asilimia sita na Samuel Sitta asilimia tano na sehemu kubwa (asilimia 24) ikienda kwa mtu yeyote atakayeteuliwa na CCM na waliosema ‘sina uhakika’ ni asilimia moja tu.
CHANZO: MWANANCHI
Ripoti hiyo inabainisha kuwa hakuna mgombea mwingine aliyepata zaidi ya asilimia 10 mwaka huu ambao ni Bernard Membe asilimia sita, Dk John Magufuli asilimia sita na Samuel Sitta asilimia tano na sehemu kubwa (asilimia 24) ikienda kwa mtu yeyote atakayeteuliwa na CCM na waliosema ‘sina uhakika’ ni asilimia moja tu.
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment