Wageni waalikwa na waandishi wa habari wakisikiliza matokeo ya utafiti
wa Twaweza kuhusu Tanzania kuelekea 2015, Dar es Salaam jana. Picha na
Edwin Mjwahuzi
Utafiti huo umebainisha kuwa kuungana kwa vyama
hivyo kutaongeza ushindani na kukitisha Chama cha Mapinduzi (CCM)
ambacho kina ngome imara. Ukawa inaundwa na vyama vya Chadema,
NCCR-Mageuzi, CUF na NLD.
Hata hivyo, takriban nusu ya Watanzania
waliohojiwa katika utafiti huo uliowataka kubainisha iwapo upinzani
ungesimamisha mgombea mmoja wangemchagua nani, walisema wangeichagua CCM
na karibu theluthi moja wangemchagua mgombea wa upinzani iwapo
watasimamisha mmoja.
Utafiti huo wa awamu ya 24 ulibainisha kuwa watu
wawili kati ya 10 walikuwa tayari kumpigia mgombea badala ya chama
wakati mmoja kati ya 10 akisema hajui angempigia nani iwapo upinzani
ungemsimamisha mgombea mmoja 2015.
“Kundi lililosema kuwa wangemchagua mgombea wa
upinzani lilipoulizwa kuwa nani anapaswa kuwa mgombea urais, watu wanne
kati ya 10 (asilimia 41) walimtaja Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod
Slaa.
“Majina mengine ya viongozi wa upinzani yaliyopata
zaidi ya asilimia 10 ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kwa
asilimia 14 na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akipata asilimia
kumi na moja.
Viongozi wengine wa upinzani waliotajwa kuwa
wangefaa kugombea urais ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto
Kabwe kwa asilimia sita huku Katibu Mkuu wa CUF ambaye pia ni Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, Mwenyekiti wa
NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema na
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, wakiambulia asilimia moja kila
mmoja.
Pamoja na mapendekezo hayo, bado karibu kila watu
wawili kati ya 10 (asilimia 21) walioulizwa swali hilo walisema hawajui
ni nani anafaa kugombea urais kupitia upinzani, jambo ambalo linaweza
kubadili matokeo hayo kwa urais katika dakika za mwisho.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment