Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camilius 
Wambura alisema jana kuwa Steven alipigwa risasi sehemu ya ubavuni 
katika eneo la Magomeni Mikumi.
Akisimulia tukio hilo, Camillius alisema Steven 
alikuwa akitoka Manzese na alipofika Magomeni Mikumi, alipigwa risasi na
 majambazi hao na kutokomea na kiasi hicho cha fedha.
Alisema tukio hilo lilitokea saa saba mchana, 
wakati Steven akiwa kwenye gari na kutakiwa kutoa fedha kabla ya kupigwa
 risasi iliyomjeruhi vibaya sehemu ya ubavu.
Kamanda Camillius alisema majeruhi amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Wambura alisema maelezo ya awali ya Steven ni kwamba alikuwa na kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kununua samani eneo la Keko.
“Kila siku tunatoa maelezo kwa wananchi kuchukua 
tahadhari wanapokuwa wamebeba fedha nyingi, lakini inaonekana imekuwa 
ngumu,” alisema Wambura.
Aliwataka wananchi kutumia mitandao ya simu 
kufanya malipo au kuomba ulinzi wa polisi wanaposafirisha fedha nyingi 
kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
“Hatari zingine ni kama za kujitakia, huwezi kuwa 
na kiasi kikubwa cha pesa kutoka sehemu moja kwenda nyingine bila kuwa 
na ulinzi,” alisema Wambura.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI

No comments:
Post a Comment