
Mkuu wa mafunzo na utendaji wa kivita,Meja Jenerali James Mwakibolwa.
Lengo la mazoezi hayo ni kubadilishana uzoefu na kuongeza ujuzi kwa maafisa ikiwa ni njia mojawapo ya kukuza uhusiano uliodumu kwa miaka mingi kati ya China na Tanzania.
Mkuu wa mafunzo na utendaji wa kivita, Meja Jenerali James Mwakibolwa, aliyasema hayo alipokuwa akizindua mazoezi hayo jijini Dar es Salaam jana na kwamba kikosi hicho maalumu kitajifunza mbinu mbalimbali za kivita na namna ya kukamata maharamia majini.
“Unajua matukio ya kiharamia katika bahari yamepungua mwaka huu ukilinganisha na mwaka jana,” alisema Mwakibolwa.
Alisema wahalifu wote waliokamatwa mwaka jana wamefikishwa katika vyombo vya sheria.
Naye Mtaalamu Mkuu wa kijeshi kamandi ya majini wa Jeshi la China, Wu Xiao Yi, alisema uzinduzi wa mazoezi hayo ni matokeo ya ushirikiano mzuri baina ya nchi hizo mbili.
“Uzinduzi wa mazoezi ya kijeshi kwa kikosi maalumu cha Marine umefungua ukurasa wa kukuza na kuendeleza uhusiano na kuboresha utendaji jeshini,” alisema.
CHANZO:
NIPASHE

No comments:
Post a Comment