Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Prof. John Nkoma.
Mfuko wa Mawasilino kwa wote (UCSAT), umeingia
mkataba na makampuni manne ya simu nchini na kampuni ya satelaiti
ya Avanti ya Uingereza, kwa ajili ya kusambaza mawasiliano kwenye kata
102 za vijijini, mtandao kwa shule za serikali 250 na kuunganisha vituo
na mafunzo ya Tehama 25.
Mkurugenzi wa UCSAT, Peter Ulanga, alisema kata hizo ni kati ya 158 zilizotangazwa, lakini kata 112 zilikubalika na kiasi cha ruzuku ni Sh. bilioni 14.2 pamoja na kata kumi za maradi wa mawasiliano mipakani ambazo zitagharimu Sh. bilioni 2.7.
Mkurugenzi wa UCSAT, Peter Ulanga, alisema kata hizo ni kati ya 158 zilizotangazwa, lakini kata 112 zilikubalika na kiasi cha ruzuku ni Sh. bilioni 14.2 pamoja na kata kumi za maradi wa mawasiliano mipakani ambazo zitagharimu Sh. bilioni 2.7.
Ulanga alisema pia mfuko huo kwa kushirikiana na makampuni hayo
wameunganisha hospitali saba na sasa wameunda kikosi kazi cha kuangalia
uwezekano wa kuunga hospitali 150 za wilaya katika huduma ya
‘telemedicine’.
Alisema pia wako katika hatua ya mwisho ya kusaini makubaliano na
Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kwa ajili ya
kugawa kompyuta mpakato kwa wanafunzi walimu ili wanaporudi kazini iwe
rahisi kufundisha wanafunzi.
Akizungumza na viongozi wa makampuni hayo, Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa, alisema awamu ya kwanza
ilihusisha kata 52, ya pili 86 na kwamba serikali inatoa zuruku nusu kwa
maeneo ya vijijini na mipakani asilimia 100 ikiwa ni utekelezaji wa
sera ya Tehama ya mwaka 2003 inayoeleza mawasiliano ni haki ya kila
mwananchi.
Alisema serikali inatambua kuwapo kwa maeneo yasiyo na mvuto
kibiashara na ndiyo maana inatoa ruzuku ya asilimia 30 hadi 80 ili
kuwezesha mawasiliano kufika. “Watanzania milioni 12.3 sawa na asilimia 57 ya wenye umri wa miaka
16 na zaidi wana akaunti za fedha za simu na asilimia 14 ndiyo wenye
akaunti benki…mawasiliano ni kichocheo cha maendeleo ya uchumi na
kijamii, yameongeza ajira kwa Watanzania 200,000 kupata ajira za moja
kwa moja, milioni 1.5 zisizo za moja kwa moja kwa makampuni hayo,”
alibainisha.
Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, John Ngodo, alisema mawasiliano
ni benki, hospitali, elimu, biashara kwa kuwa yanarahisisha na kuwezesha
utoaji wa huduma ya kusaidia kukuza uchumi kwa kasi kubwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Prof.
John Nkoma, alisema jamii inapaswa kutumia vizuri mawasiliano na mtandao
kwani kwa siku za hivi karibuni licha ya kuwapo kwa kasi ya mawasiliano
pia kuna kasi ya matumizi mabaya ya mtandao.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment